
Kikosi cha klabu ya KMC cha msimu uliomalizika wa mwaka 2020-2021.
KMC FC inawajulisha mashabiki, wapenzi na Watanzania kwa ujumla kuwa usajili unaoendelea kufanyika umezingatia matakwa ya mwalimu na kwamba inasajili wachezaji wenye viwango vya hali ya juu na bora watakaoleta manufaa makubwa katika timu hiyo.
Ikumbukwe kuwa Klabu ya KMC FC imeanza rasmi kambi mkoani Morogoro kwa ajili ya kujiandaa vizuri na msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania Bara 2021/2022 tokea Agosti 26 mwaka huu baada ya kuwasili mkoani humo asubuhi ya Agosti 25, 2021.
KMC FC ikiwa mkoani humo kwa maandalizi hayo ya msimu mpya itakuwa na programu mbalimbali za mazoezi pamoja na kucheza mechi za kirafiki kama program inavyoonyesha kwa lengo la kuwapima na kuwaweka vizuri wachezaji kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu itakayoanza Septemba 27 mwaka huu.