
Mlinda mlango wa zamani wa Yanga, Farouk Shikalo akiwa mazoezini
Shikalo amejiunga na KMC ikiwa ni siku chache baada ya kuachwa na Yanga ambayo iliweka wazi kuwa isingendelea kufanya kazi na kipa huyo raia wa Kenya baada ya Mkataba baina ya pande hizo mbili kumalizika.
Nyota huyo aliitumikia Yanga kwa misimu miwili lakini alijikuta akipoteza namba mbele ya Metacha Mnata ambaye pia aliachwa na wanajangwani hao baada ya Mkataba wake pia kumalizika.
Kipa huyo ataungana na mkongwe Juma Kaseja katika kupigania namba kwenye kikosi cha KMC ambacho kinanolewa na Kocha Habibu Kondo.