Tuesday , 2nd Nov , 2021

Zoezi la ugawaji wa taulo za kike katika kampeni ya Namthamini mwaka 2021 limekamilika katika mkoa wa Kigoma. 

Wanafunzi wa Kigoma Grand Sekondari wakifurahi baada ya kupokea taulo za kike

Jumla ya shule 6 za mkoa huo zimenufaika na mchango, tatu kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na zingine tatu kutoka Halmashauri ya Kasulu Mji, ambapo wanafunzi 600 wamepokea taulo za kike kwa mwaka mzima. 

Shule nufaika za Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ni Katubuka Sekondari, Mwananchi Sekondari na Mlole Sekondari na zilizonufaika kutoka Halmashauri ya Kasulu Mji ni Kigoma Grand Sekondari, Bogwe Sekondari na Murubona Sekondari. 

Ndani ya mwaka 2021, kampeni ya Namthamini imefanikiwa kugawa taulo za kike kwa wanafunzi 1400 kwa mwaka mzima katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Kigoma.