Monday , 6th Dec , 2021

Kampeni ya Namthamini imekamilisha zoezi la ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule mbalimbali wenye uhitaji kwa mwaka 2021 katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Ugawaji wa taulo za kike wilayani Bagamoyo

Shule iliyonufaina na msaada huo ni Shule ya Sekondari ya Matimbwa iliyopo nje kidogo ya Mji wa Bagamoyo, ambapo jumla ya wanafunzia 100 wamepatiwa taulo za kike kwa mwaka mzima.

Akizungumza kwa niaba ya serikali, Afisa Elimu, anayeratibu masuala ya Afya, Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Sophia George Killumbi, amesema, "Taulo hizi za kike zitakuwa ni msaada sana kwetu na kwa niaba ya serikali niwakaribishe wilayani kwetu wakati mwingine"

Ndani ya mwaka 2021, kampeni ya Namthamini imefanikiwa kugawa taulo za kike kwa wanafunzi 1500 wa shule mbalimbali kwa mwaka mzima katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Kigoma na Pwani.