
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro.
Taarifa hiyo imetolewa hii leo Desemba 23, 2021, na Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo Jumanne Muliro.
"Waliokamatwa miongoni mwao ni watuhumiwa saba, ambapo kundi hili yumo mtuhumiwa anayeitwa Yohana Zacharia maarufu kama Cobra, yeye na wenzake wamekuwa wakitumia bastola bandia kutishia watu na kunyang'anya vitu Mabwepande, Ulongoni na Banana," amesema Kamanda Muliro.