Monday , 27th Dec , 2021

Bondia Erick Tshimanga Katompa amepinga matokeo ya sare dhidi ya bondia Mtanzania, Selemani Kidunda kwenye mpambano uliotazamiwa kuwa wa mzunguko wa kumi kuwania mkanda wa WBF 2021 uliofanyika usiku wa jana Disemba 26, 2021.

(kutoka kushoto: Kidunda, Promota Selemani Semunyu na Katompa)

Katompa amepinga matokeo hayo kwa kusema kuwa mpinzani wake Kadunda angeweza kutibiwa na kurejea ulingoni kuendelea na mpambano na si mwamuzi kuamuru kuvunja pambano na kutoa matokeo ya sare.

Hayo yalijiri baada ya bondia Katompa kutoka DR Congo kumchezea mchezo usio wakiungwana Kidunda kwa kumpiga kichwa jambo lililopelekea Kidunda achanike sehemu yake ya jichoni na kushindwa kuendelea na pambano.

Sheria za IBF zinawalazimu kutoa matokeo ya sare kwasababu tu tatizo hilo limejitokeza katika raundi ya tatu lakini Kidunda angeweza kupewa ushindi endapo pambano hilo lingefika mzunguko wan ne.

Bondia Kidunda yeye amemlaumu Katompa kwa kumsababishia jeraha hilo kwa makusudi na kusema kuwa amemchafulia rekodi yake kwani hajawahi kutoka sare katika mapambano yake. Pambano hilo lilikuwa la raundi kumi.