Monday , 3rd Jan , 2022

Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC imemtangaza Mwanahabari Ahmed Ally kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo.

Simba SC imemtangaza Ahmed ambaye alikuwa Mtangazaji wa Azam Media, akichukua nafasi ya Haji Manara ambaye aliondoka klabuni hapo mwaka 2021.

Hata hivyo Mashabiki na Wanachama wa Simba SC walitarajia utambulisho wa mchezaji mpya kufuatia maelezo yaliyowekwa kabla kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za klabu hiyo.

Taarifa iliyowekwa awali kwenye kurasa za Simba SC ilisomeka: "Baada ya kumsubiri kwa muda hatimaye kijana wetu Amefika"