Tuesday , 18th Jan , 2022

Wananchi wa kijiji cha Mkwanga halmashauri ya wilaya ya Kigoma wanalazimika kuendelea kutumia maji machafu ya mto Kaseke baada ya mkandarasi anayesimamia na anayetekeleza mradi wa maji katika eneo hilo kushindwa kukamilisha maboresho ya mradi huo uliotakiwa kukamilishwa mwezi Mei 2021.

Wananchi wakichota maji ya mto Kaseke

Mkandarasi anayesimamia mradi wa maji kijijini hapo anaitwa Howard Consulting Company na anayetekeleza ni Serengeti Company Limited kushindwa kukamilisha kwa wakati kwa zaidi ya awamu mbili sasa.

Wananchi wa kijiji hicho wamesema wanalazimika kutumia maji hayo ambayo ni machafu kutokana na kutokuwa na mbadala wa maji mengine hivyo kuomba hatua za haraka kuchukuliwa ili kunusuru afya zao.