(Baadhi ya Waamuzi wa Ligi Kuu NBC Tanzania 2021-2022)
Semina hiyo inataraji kumalizika Alhamisi ya Februari 17 mwaka huu ikiwa ni semina iliyopo kwenye utaratibu wa kawaida kwa TFF kuendesja Semina kwa waamuzi kila msimu kwa lengo la kuwajengea uwezo waamuzi hao na Uadilifu.
Lawama kutoka wadau mbalimbali na baadhi ya wapenzi wa soka zimekuwa nyingi hadi kupelekea Waziri mwenye dhamana ya Michezo, Mh. Mohammed Mchengerwa kutoa agizo TFF na Baraza la Michezo nchini BMT kulishughulikia changamoto hizo.
Vile vile, Waziri Mchengerwa ameitaka Taasisi ya Kuchunguza, Kupinga na Kupambana na Rushwa TAKUKURU kushiriki katika kuchunguza harufu za Rushwa ambazo zinazungumzwa bila kuthibitika.
Waziri Mchengerwa amesema kuna waamuzi 13 wamoendolewa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi kuu jambo ambalo halikumfurahisha na kumfanya kujiuliza swali ya kuwa, mpaka kufikwa kwa mwisho wa ligi watakuwa wamesimamwa wangapi?

