Wednesday , 20th Apr , 2022

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, amesema kuwa endapo nchi yake ingekuwa inamiliki silaha bora zaidi ikilinganishwa na zile za Urusi, basi wangekuwa tayari wamekwishamaliza vita nchini humo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky

Rais Zelensky alisema hayo katika mahojiano yake na majadiliano na viongozi wa mataifa yaliopiga hatua kubwa kidemokrasia na kuongeza kwamba iwapo Taifa lake lingefanikiwa kupata silaha hizo ambazo wameahidiwa wiki zijazo, zingesaidia kuokoa maisha ya maelfu ya watu.

"Hatma ya makumi ya maelfu ya wakaazi wa Mariupol ambao walipelekwa katika maeneo yanayodhibitiwa na Urusi haijulikani", amesema Zelensky.

Rais ameongeza kwamba uwezo wa mashambulizi ya Urusi katika maeneo ya Kharkiv, Donbasna Dnipropetrovsk umeongezekana hata kulenga makaazi ya raia.