Wednesday , 20th Apr , 2022

Msanii Ten Ballz kutoka 254 Kenya amesema ataongea na wahusika wa soko la muziki wa Kenya kama wanaweza kumvuta msanii wa filamu Steve Nyerere kuwa msemaji wao.

Picha ya msanii wa filamu Steve Nyerere

"Nitaona kama nitaongea na wahusika wa Industry ya Kenya kama tunaweza kumvuta. Acha aje Kenya tuna pesa, akija kuongea kuhusu muziki wetu fresh kwa sababu hatuna muongeaji" amesema Ten Ballz 

Steve Nyerere alichaguliwa kuwa msemaji wa shirikisho la muziki Tanzania lakini akajiuzulu kutokana na kupingwa na wasanii ambao wanadai hafai kuwa kwenye nafasi hiyo.

Zaidi tazama hapa kwenye video.