Monday , 2nd May , 2022

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Abdallah Pazi 'Dullah Mbabe' amewasili mkoani Ruvuma tayari kwa pambano lake maalum la Kimaonyesho linalotarajia kupigwa leo Jumanne katika Wilaya Tunduru.

ondia wa ngumi za kulipwa nchini, Abdallah Pazi 'Dullah Mbabe'

Dullah Mbabe atapanda ulingoni kwenye pambano hilo litakalopigwa kwenye Uwanja wa CCM Wilaya hapa Tunduru mkoani Ruvuma ikiwa na lengo la kuhamasisha ngumi mkoani hapa pamoja na kupata  mabondia watakaopanda ulingoni katika pambano la Seleman Kidunda dhidi ya Tshimanga Katompa ambalo linatarajia kupigwa Julai 30, mwaka huu Songea, mkoani 

 Akizungumza mara baada ya kuwasili Tunduru ambapo amepokelewa na shangwe la mashabiki waliokuwa wakimsubiri kwa hamu kutokana na kumuona katika luninga wakati wa mapambano yake, alisema kuwa hakutegemea kama angeweza kupokelewa kwa shangwe ambalo amelipata kutoka kwa mashabiki hao hivyo ana deni kubwa kwao kwa kuwaonyesha mchezo mzuri katika pambano lake la leo dhidi ya Ramadhan Migwede.

"Kwanza namshukuru Mungu nimeweza kufika salama hapa Tunduru, safari ilikuwa ndefu sana japo njiani imenifanya kuona ukubwa wa mashabiki wangu hasa kwa mikoa hii ya kusini, kwangu ni jambo zito ambalo sikulitarajia hapo awali.

" Nimekuja kucheza katika hili pambano kwa lengo la kuhamasisha ngumi hapa kwa sababu ngumi zinapaswa kuwa na nchi yote siyo baadhi ya mikoa, namshukuru promota kwa wazo hili ila niwaombe mashabiki wangu wa hapa Tunduru mje kwa wingi kuangalia burudani kutoka kwangu," amesema  Dullah Mbabe.

Mabondia hao wanatarajia kupanda ulingoni kwenye pambano hilo linalotarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Wilaya ya Tunduru kwa kuwakutanisha Chidy Benga wa Songea dhidi ya Yazidu Khalfani wa Tunduru wakati Matumla Matumla wa Tunduru akitarajia kumvaa Azizi Azizi wa Songea.

 Wengine ni Karim Mwenda wa Songea atakayecheza na Giliki Giliki wa Tunduru wakati Bashiru Kazembe atacheza na Kapinga, Seleman Khalifa vs Judi Rajabu, Julo Julius vs Mwakinyo Mbabe wote wakiwa ni wa Tunduru wakati  Kachala Mnyama yeye atacheza dhidi ya Junior kutoka Malawi.