
Afisa wa Ushirika Wilaya hii ya Meatu, Masanja Shilabu, mbele ya Wajumbe wa Baraza la Madiwani walioketi Mjini Mwanhuzi, ametangaza uamuzi huo huku akisema katika wilaya ya Meatu kuna vyama vya AMCOSS 73 na kati ya hivyo 14 vimechukuliwa hatua ikiwemo hatua hiyo ya kuwafuta kazi watumishi hao.
Wakati hayo yakijiri, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Dakawa Juma Msoleni, amesema zaidi ya watumishi 800 wamefanikiwa kulipwa mapunjo ya mishahara yao, na amewataka kuzidisha morali ya kazi zao.
Msoleni amesema watumishi wote wa Halmashauri ya Meatu wanalazimika kufanyakazi kwa bidii na maarifa zaidi, ili kufikia lengo la kuongoza kimapato nchini ifikapo mwaka 2023.