Sunday , 8th May , 2022

Kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika nchi nyingi, Muungano wa mashirika ya ndege nchini Nigeria umesema utasimamisha safari zote za ndege kuanzia kesho Jumatatu Mei 9/2022.

Bei ya mafuta ya ndege imepanda kutoka Naira 190 za Nigeria hadi Naira 700 kwa lita bei ambayo wanadai hawawezi kuimudu

Wizara ya usafiri wa anga imeutolea mwito muungano huo kuzingatia athari za kusitisha safari za ndege kwa Wanigeria na wasafiri wa kimataifa.