
Zlatan Ibrahimovic(kushoto) na aliyekuwa wakala wake marehemu Mino Raiola(kulia) enzi za uhai wake.
Zlatan mwenye umri wa miaka 40 ambaye ameisadia Ac Milan kutwaa ubingwa walipoifunga Sassoulo 3-0 jana, amesema ni taji lake la kwanza analoshinda bila ya uwepo wa Mino karibu yake .
AC Milan ilitwaa ubingwa huo waliousubiri kwa muda mrefu na jana walifikisha alama 86, wakifuatiwa na Inter Milan waliomaliza msimu kwa ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Samdoria na kufikisha alama 84 ambazo hazikutosha kuutetea ubingwa.
Mabao ya AC Milan yaliwekwa kimiani na mshambuliaji hatari Olivier Giroud aliyefunga mara mbili na Franck Kessie huku kinda Raphael Leao akitengeneza nafasi zote hizo za mabao.
Mara ya mwisho kutwaa ubingwa wa Serie A ilikuwa ni mwaka 2011 walipokuwa wakinolewa na Maximilliano Allegri na tangu hapo makocha wengi walishindwa kupeleka furaha katika kikosi hicho wakiwemo Clarence Seedorf,Philipo Inzaghi,Vincenzo Montella,na Gennaro Gattuso .
Napoli ilishinda bao 3-0 dhidi ya Spezia na wakamaliza katika nafasi ya tatu nayo Juventus ikamaliza katika nafasi ya nne.