Friday , 22nd Jul , 2022

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa onyo kwa baadhi ya wananchi wanaoshiriki katika uharibufu wa miundombinu ikiwemo barabara nchini na kuwataka watanzania kulinda miundombinu hiyo

Kauli huyo ameitoa wakati akifungua barabara ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass) yenye urefu wa kilomita 42.4.

"Kumeanza kujitokeza vitendo vya kuharibu miundombinu yetu, tunaona Jeshi la Polisi wakizungumzia jinsi ya kutunza barabara zetu na kutokutengeneza magari yanayoharibika barabarani"

"Suala za kuzidisha uzito wa magari yetu na lenyewe linakwenda kuharibu barabara zetu, kutupa taka kwenye madaraja na kuchimba mchanga, niwaombe sana wananchi kufuata taratibu zilizowekwa ili tutunze miundombinu yetu" amesema Rais Samia

Katika ufunguzi huo umehudhuriwa na marais wa nchi za Jumuiya ya afrika Mashariki ambao wapo mkoani Arusha kwa ajili ya mkutano wa kawaida wa Jumuiya hiyo