Friday , 22nd Jul , 2022

Mkuu wa mkoa wa Mara Ally Hapi, amewaonya baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakiyawezesha makundi ya vijana kuvamia na kupora mawe ya madini ndani ya mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara.

Mkuu wa mkoa wa Mara Ally Hapi

Ameyasema hayo wakati alipotembelea mgodi wa dhabu wa Barrick North Mara na kukuta malalamiko ya uvamizi wa mara kwa mara unaotoka kwa wakazi wanaozunguka mgodi huo hasa kijiji cha Makerero ambapo aliuambia mgodi huo kuona haja ya kulipa fidia kwa wakazi hao ili kuepusha wizi unaojitokeza kila wakati.

"Haiwezekani mtu anakamatwa kaiba mgodini anahukumiwa kifungo lakini anaonekana mtaani, hapa kuna mapapa ambao wao ndio wanadhamini uhalifu huu, kama tuliweza kuwabaini mapapa kwenye uthamini na tukaokoa bilioni 20 tutashindwaje kuwabaini hawa mapapa wanaowafadhili hawa maintuda," amesema RC Hapi

Kwa upande wa kamanda wa Polisi wa Tarime, Rory Godfrey Sarakikya, amesema yawezekana wafanyakazi ambao wapo ndani ya mgodi nao wakawa wanachangia katika utoaji wa taarifa za uwepo wa mawe ya madini.