Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na na Teknolojia Prof.Aldof Mkenda Jijini Dodoma kwenye mkutano wa wadau ambao walikua wanajadili na kutoa maoni juu ya Rasimu ya Sera ya Sayansi ,Teknolojia na ubunifu na kiunzi cha Uratibu wa Ubunifu nchini,ambapo tayari wanafunzi 600 wameshaanza kujiandikisha ili kupata ufadhili huo.
Alisema kuwa wote ambao watahitimu chini ya Samia Scholarship watakua na uwezo wakuomba mkopo na watapatiwa ili kujiendeleza kimasomo.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia alisema Nchi nyingi duniani zinazoendelea ni zile ambazo zinategemea ubunifu zaidi katika utafutaji maendeleo ya wananchi wake kwakua ubunifu ni nguzo kubwa hivyo ni vyema kuwekeza kwenye Elimu.
Prof.Mkenda alisema swala la elimu ni namba moja kwa nchi nyingi duniani kwakua kupitia elimu inapatikana Teknolojia na ubunifu ndio maana Serikali inakutana na wataalamu wa elimu kutoka sehemu mbalimbili ili kubadilisha ujuzi na maoni yakuangalia ni namna gani mitaala iendane na soko la ajira kidunia na pia kuhakikisha Elimu inatoa ujuzi kwa wahitimu.
Prof.Mkenda alisema Serikali haitaki kukurupuka katika kufanya maboresho ya elimu kwakua elimu ndio dira inayoonyesha maisha ya muhitimu na katika ushindani kwa soko la kimataifa ndio maana wanatumia muda mrefu kufanya maboresho ya elimu.

