
Baadhi ya makazi ya watu Somalia
Akizungumza hii leo Mkuu wa kitengo kinachohusika na masuala ya binadamu Martin Griffiths, ametoa tahadhari hiyo katika Mji Mkuu wa Mogadishu, na kwamba njaa kali inatarajiwa kuyamkumba maeneo kadhaa ya katikati Kusini mwa Somalia ndani ya mwezi Oktoba mpaka Desemba mwaka huu.
Ametoa angalizo hilo wakati alipofanya ziara kusini magharibi mwa nchi hiyo kwenye maeneo ya Baidoa , eneo mbalo limeathiriwa vibaya na ukame.
Kutokana na mvua kukwama kunyesha ndani ya misimu minne, jiji hilo limekua na ukiwa huku watu wakipoteza kila kitu sababu ya ukame mkubwa na ikikadiriwa kwamba zaidi ya watu milioni 1 wameyakimbia makazi yao.
Janga hilo linasemekana kuwa kubwa zaidi kuwahi kutokea ndani ya miaka 40 iliyopita na kwamba Umoja wa Mataifa ukisema kuwa takribani watu milioni 22 wapo hatarini kufa njaa.