Monday , 10th Oct , 2022

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera  amewataka viongozi wa  Halmashauri zote za mkoa huo kumpatia taarifa za watumishi watakaotumia fedha za lishe kinyume na maelekezo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ametoa kauli hiyo wakati wa zoezi la utiaji saini wa mkataba wa Afua za lishe ambao una lengo la kutoa elimu kwa wananchi ili kukabiliana na tatizo la udumavu uliosainiwa na  wakurugenzi na wakuu wa Wilaya.

Mratibu wa lishe  Mkoa wa Mbeya, Benson Sanga amesema mkoa umetenga kiasi cha sh milioni 400 kutekeleza Afua mbalimbali za lishe katika kipindi cha mwaka 2022 huku Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Ezekiel Maghehema akielezea utekelezaji huo.