Thursday , 13th Oct , 2022

Leo Oktoba 13,2022 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetaja kesi ya madai, iliyofunguliwa na Patrick Christopher Kamwelwe, dhidi ya Willium Malecela na aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Paul Makonda

Patrick (Mdai) amewasilisha mahakamani madai yake ya kwamba alikuwa akimiliki gari aina ya Range Rover ambalo alimkabidi Willium Malecela maarufu kama Lemutuz, ambaye naye alidai kuwa gari hiyo alikabidhi Makonda alitumie kwa wiki mbili, lakini gari hiyo halikurudishwa kwa mmiliki hadi leo.

Kesi hiyo ambayo imetajwa kwa mara ya kwanza mbele ya Hakimu Mkazi Richard Kabate, imeahirishwa hadi Novemba 8, 2022, itakapotajwa tena.