
Hamad Chande, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango akipokea msaada
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande kwaniaba ya serikali anapokea msaada wa vifaa kinga dhidi ya UVICO 19 kutoka Benki ya Msaada wa Maendeleo na Biashara ya kusini na Mashariki mwa Afrika chini ya COMESA, na kwamba msaada huu utasaidia wataalam waliopo mipakani kujikinga pia na Ebola iliyoripotiwa nchi jirani.
"Msaada huu ambao tumeupokea leo kwa niaba ya serikali ilitiwa saini Januari 2022, ni msaada mkubwa wa vifaa kinga kwa serikali ya Tanzania na umekuja wakati mwafaka kwamba mbali na lengo lake la UVICO 19 lakini kuna mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchi jarani, hivyo tutaumia kuhakikisha hata wataalam wetu wa afya mipakani wanakuwa na vifaa kinga hivi ili kujiweka salama. Benki hii sisi ni wanahisa wake kwasababu tupo kwenye Jumuiya ya Soko Kuu la Kusini na Mashariki mwa Afrika ( COMESA) na nchi imenufaika mno kuwa mwnachama wa COMESA"- Hamad Chande, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango.
Aidha, akizungumza kwa niaba ya wizara ya Afya, Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Seif Shekalaghe ameahidi kuvitumia kwa usahihi huku mwakilishi wa TDB akisema kuwa wataendelea kutoa misaada ya maendeleo kwa Tanzania.