Sunday , 16th Oct , 2022

Kufuatia uwepo kwa heka heka za ulinzi shirikishi katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam balozi wa nyumba hamsini mtaa wa magomeni Ramadhani Bwanga amesema kuna mitaa ambayo zoezi hili la ulinzi shirikishi limekuwa la kisiasa.

Akizungumza na EATV amesema kwamba hali inapelekea ulinzi na usalama kuacha misingi ya kuwatumia mabalozi.

‘Katika eneo letu tunaonekana kama hatujajipanga, pia tunakwamishwa na watu wenye mamlaka ambao wanachangia mambo yasikae sawa, huu mtaa upo mjini na kuna maduka ya kutosha na hayo maduka yana walinzi’

Amesema Bw. Ramadhani na kuongeza kuwa Tunakosa nguvu maana tukipeleka mawazo yetu kwa viongozi wa juu hayafanyiwi kazi.’

Amesema zamani huko balozi wa shina alikuwa akijua nyumba ipi kuna mgeni na utaratibu mzima lakini kwa sasa mambo ymekuwa ndivyo sivyo huku chibni mabalozi hawapewi ushirikiano wa kutosha hali inayosababisha ulinzi kuwa na changamoto za usalama.