
Katika mkutano wake na wanahabari kwa njia ya mtandao balozi huyo amesema kuwa upo ushuhuda wa wazi wa faida za uwekezaji nchini Burundi huku akiweka wazi kuwa zipo kampuni 13 za watanzania ambazo zimewekeza nchini Burundi
"Fursa za uwekezaji ni nyingi na wawekezaji hawatajutia, ushuhuda wa faida ya kuwekeza Burundi upo maana tuna wawekezaji kutoka Tanzania ambao wapo hapa kwa muda na wamekuwa wakifanya vizuri, kuna makampuni takribani 13 ya Kitanzania yamewekeza Burundi" amesema Balozi Maleko
Katika fursa nyingine Balozi huyo amesema kuwa Burundi kuna soko kubwa la bidhaa kutoka Tanzania ikiwemo matunda kama maparachichi na zao la mchele kwa kuwa bidhaa za Tanzania zinapendwa sana Burundi
"Bidhaa ambazo Tanzania inazinunua kutoka Burundi ni pamoja na matunda hususani maparachichi na mwaka jana Tanzania tuliongoza kwa kununua maparachichi kutoka Burundi
"Mchele wa Tanzania unapendwa hapa Burundi, kwa mfano mwaka 2021 Burundi ilinunua mchele wenye thamani wenye thamani ya dola za Marekani milioni 7.9 kutoka Tanzania" amesema Balozi Maleko
Katika hatua nyingine Balozi Maleko amesema kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya umeme nchini Burundi ikiwemo Viwanda na ujenzi wa miundombinu Tanzania inaweza kutumia fursa hiyo kuuza umeme nchini humo pindi bwawa la mwalimu Nyerere litakapokamilika
"Serikali ya Tanzania ina fursa ya kuuza umeme Burundi, kwa sababu Burundi ina mahitaji makubwa ya umeme, kwa sababu kuna ongezeko kubgwa la shughuli za kiuchumi kama viwanda na ujenzi wa vitu mbalimbali,tutakapoanza kuzalisha umeme tunaweza kutumia hiyo fursa "