Thursday , 3rd Nov , 2022

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima ametoa siku saba kwa viongozi  wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa huo kufanya opereshi na kuwakamata waliohusika na mauaji ya Joseph Mathias mwenye umri  wa miaka 50 mkazi wa Kijiji cha Ngulla Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza ambae ni mlemavu wa ngozi

Joseph ameuwawa kwa kukatwa panga  na watu wasiojulikana kwenye mkono wake wa kulia  usiku wa kuamkia leo Novemba 3/2022 akiwa nyumbani kwakwe.

Inaelezwa kuwa watu hao ambao idadi yao bado haijafahamika walivamia nyumba aliyokuwa akiishi Joseph Mathias na familia yake na kisha kutekeleza mauaji hayo

Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu mkoa wa Mwanza Alfred Kapole amesikitishwa na tukio hilo na kuiomba jamiii kuacha kufanya vitendo vya kikatili

kwa upande wake Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Mairi Makori amesema hadi Sasa tayari wanawashikilia watu watatu katika tukio hilo.