Thursday , 17th Nov , 2022

Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mette Norgaard Dissing-Spandet, amesema nchi yake itaendelea kushirikiana na serikali sambamba na mashirika ya kijamii  katika utoaji wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana na stadi za maisha ambazo zitawasaidia kujiendeleza kiuchumi kwa kujiajiri.

Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mette Norgaard Dissing-Spandet

Balozi huyo ametoa kauli hiyo wakati wa maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa klabu za FEMA  ambazo zimekuwa zikiwapa vijana nafasi ya kujitanbua sambamba na kuwapa stadi ambazo zinawasaidia kufanya maamuzi mbalimbali katika maisha yao na kufikia malengo katika maisha yao

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkurugenzi wa shirika la Femina Amabilisi Batamula, amesema kupitia programu mbalimbali za klabu za Femi vijana wameonyesha kufikiwa na elimu ya virusi vya ukimwi kwa kupata taarifa sahihi na Kwa sasa wanawaemisha namna ya kutengemeza kipato lakini pia kujitoa katika kuleta mabadiliko kwenye jamii zao

Nao baadhi ya vijana walionufaika na Femi klabu wameeleza jinsi walivyonufaika na kusaidiwa katika masuala ya elimu ya afya ya uzazi na virusi vya ukimwi hadi kufikia kujiajiri wao wenyewe kutokana na baadhi yao kutamani hata kuacha masomo yao na kuingia kwenye fani ya uimbaji nyimbo za bongo fleva