Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Viwanda vya Misitu Tanzania (FITI)
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Juma S. Mkomi, mkoani Kilimanjaro, alipokuwa akizungumza na wahitimu na wageni mbalimbali waliohudhuria mahafali ya 25 ya chuo hicho.
Amesema sekta ya misitu ina fursa nyingi kuanzia kwenye uhifadhi hadi utumiaji wa mazao ya misitu, hivyo wahitimu hao ni vyema wakatumia taaluma waliyoipata kuchangamkia fursa zilizopo kutengeneza ajira kwa faida yao wenyewe na jamii kwa ujumla.
Katika hotuba yake amewasisitiza wahitimu hao wawe wazalendo na waadilifu watakapokua wakitekeleza majukumu yao huku akitoa wito kwa bodi ya ushauri ya chuo hicho iendelee kuishauri menejimenti ya FITI kutoa mafunzo kwa kuzingatia miongozo ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na ya Ufundi Stadi (NACTVET).
Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) kilianzishwa mwaka 1976 kikiwa na jukumu la kutoa mafunzo ya teknolojia ya viwanda vya misitu kwa ngazi ya cheti na diploma pamoja na mafunzo ya muda mfupi ya uvunaji wa miti, uchakataji wa magogo, usimamizi wa viwanda, ushauri na utafiti kuhusu usimamizi.