
Nyumba ambayo imekutwa na mwili
Imedaiwa kuwa huenda kifo hicho kimetokea siku kadhaa zilizopita kutokana na mwili huo kukutwa umeharibika.
Akizungumza kwa njia ya simu Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa, amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa bado jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini undani wa kifo hicho.
Kaimu Mganga Mfawidhi hospitali ya wilaya Manyoni Dkt. Ainea Mlewa, amekiri kupokea mwili huo ambao umehifadhiwa katika chumba cha kuhidhia maiti.