Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,
Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 23, 2022, mkoani Manyara, wakati akizungumza na wananchi wakati akihitimisha ziara yake za siku mbili mkoani humo.
"Nataka niwahimize, tulime kwa sababu miaka ijayo Dunia inaona hatari ya njaa, balaa la nja dunia nzima, Tanzania hatuna sababu ya kulia njaa na ndiyo maana tunaweka miundombinu ya kuzalisha mbegu, tunajenga miundombinu ya kumwagilia na tumeanza kilimo cha mashamba makubwa ili tulime kwa wingi," amesema Rais Samia
Aidha Rais Samia ameongeza kuwa "Tuweke akiba ya kutosha (akiba ya chakula) na tuwauzie majirani zetu, Tanzania Mungu ametupendelea ardhi nzuri, maji tunayo, mvua inanyesha kwa wakati wake la maana ni kukinga maji ya mvua na kuyahifadhi ili yatumike kwenye kilimo na kwenye matumizi mengine,".