
Wahudumu wa afya
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki, amesema hiyo ni fursa kubwa na unafuu kwa wafanyabiashara na wanafunzi wanaoenda nchini humo.
"Habari njema kwa wasafiri wanaokwenda China- kuanzia tarehe 8 Januari 2023 hakuna tena sharti la kukaa karantini siku 8, wasafiri wanachotakiwa ni kupima uviko19 masaa 48 kabla ya safari, hatua hii italeta unafuu mkubwa kwa wanafunzi na wafanyabiashara wanaokwenda China," ameandika Balozi Kairuki