
Hayo yamesema na msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP David Misime ambapo amewaomba wazazi kushirikiana na Jeshi hilo kuwalinda watoto
Ameongeza kuwa madereva wa vyombo vya moto wazingatie utamaduni unaosisitizwa na Jeshi hilo wa kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani na kujiepusha na matendo yatayohatarisha usalama wa watoto wanaorudi mashuleni
SACP Misime amewaonya baadhi ya madereva kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuwaumiza watoto kimwili na kisaikolojia.