Monday , 16th Jan , 2023

Kasisi mmoja wa Kanisa Katoliki ameuawa na watu wenye silaha katika parokia yake kaskazini mwa Nigeria,  huko katika  jimbo la Niger.

Wauaji hao pia walichoma moto makazi yake  na baadae kutekeleza mwili wa Padri huyo kwenye   magofu. 

Tukio la kuuawa kwa Padri Isaac Achi limejiri jana asubuhi  katika shambulio ambalo Padri mwingine, Padri Collins Omeh, alipigwa risasi alipokuwa akijaribu kutoroka na baadaye kupelekwa hospitalini.

  Padri Achi aliuawa kwa kupigwa risasi na watu hao wenye silaha, ambao alisema walikuwa wakipiga kelele za jihadi.

Katika tukio jingine, genge moja katika jimbo la kaskazini magharibi la Katsina liliwateka nyara watu wasiopungua watano walipokuwa wakijiandaa kufanya  ibada kanisani.

Nigeria imekuwa ikipambana na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Boko Haram - na makundi yake  kwa zaidi ya muongo mmoja. Wapiganaji wake wamewalenga Wakristo na Waislamu katika kipindi hicho.