Wednesday , 18th Jan , 2023

Mfanyakazi wa TANESCO mkoani Songwe Angel Shakinyao (33), amefariki dunia baada ya kunyongwa kwa kamba iliyochanywa kwenye bajaji na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Januari 16, 2023, wakati akirudi nyumbani na mwili wake kutupwa jirani na nyumba anayoishi.

Picha ya Angel Shakinyao (33)

Mkuu wa mkoa wa Songwe Waziri Kindamba, ameliagiza jeshi la polisi mkoani humo kuwasaka na kuwakamata watu wote waliohusika katika mauaji hayo.

Akitoa salamu za pole Mkuu wa mkoa wa Songwe Waziri Kindamba, amewataka wananchi kuwa na utulivu wakati jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi.

Mwili wa Angel umeagwa katika makazi yake mjini Vwawa na kusafirishwa kwenda mkoani Dodoma kisha kupelekwa nyumbani kwao shinyanga kwa ajili ya mazishi.