Saturday , 25th Feb , 2023

Mgombea urais wa chama tawala cha APC nchini Nigeria , Bola Tinubu, ameshinda katika matokeo ya awali kitengo chake cha kupigia kura mjini Lagos.

Awali kulikuwa na matukio ya kutatanisha mapema wakati vyombo vya habari vilipojaribu kupata picha za Bw Tinubu alipokuwa akipiga kura yake.

Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:

APC - 33

LP - 8

PDP - 1

YPP – 1

Wagombea watatu wanaonekana kuwa mstari wa mbele kumrithi Rais Muhammadu Buhari. Wanaowakilisha vyama viwili vikubwa vya kisiasa ni Bola Tinubu na Atiku Abubakar. Mwingine, Peter Obi, ambaye anaungwa mkono hasa na vijana katika maeneo ya mijin