Friday , 3rd Mar , 2023

Wagonjwa wanaofuata matibabu katika hospitali ya Consolatha Ikonda wilayani Makete mkoani Njombe, wameilalamikia serikali kuzuia kituo cha mabasi cha Ikonda kutumika  na badala yake watumie kituo kipya cha Tandala ambacho ni mbali na hospitalini na kusema marufuku hiyo imeongeza usumbufu

Wagonjwa

na kuweka hatarini usalama wa wagonjwa wenye hali mbaya.

Kufuatia katazo hilo lililokuja punde baada ya halmashauri kuanzisha mradi wa kituo kidogo cha Tandala kilichopo mbali na hospitalini  Ikonda ,kinawaibua wagonjwa na abiria wengine wanaofata matibabu wanasema maisha yao yamekuwa hatarini hasa nyakati za usiku kwa sababu wanalazimika kupanda pikipiki na wagonjwa mahututi huku wengine wakikiri kuzurumiwa fedha na bodaboda.

Akifafanua sababu ya kupiga marufuku matumizi ya kituo cha mabasi cha Ikonda Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete William Makufwe, amesema ni kuiweka mbali stendi na hospitali na kwamba kinachokwenda kufanyika ni kuboresha usafiri wa wagonjwa.  

Hospitali ya Consolata Ikonda imekuwa kimbilio la wagonjwa kutoka maeneo tofauti ya Tanzania kutokana na huduma zake ambapo inakadiriwa zaidi ya wagonjwa 300 hufika kupata tiba kwa siku  katika hospitali hiyo.