Huduma za dharura zinasema ajali hiyo ya usiku wa kuamkia leo ilitokea baada ya treni iliyokuwa ikisafirisha takriban watu 50 kugonga hema la ujenzi .
Treni ya mizigo pia imeripotiwa kuharibiwa.Baadhi ya watu walitibiwa katika eneo la tukio, lakini 19 wamepelekwa hospitalini.Wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakiwahudumia abiria hao wenye majeraha madogo.
Ajali hiyo imesababisha uharibifu wa kuibomoa treni na kushusha moja ya nyaya za umeme wa juu. Sehemu kubwa ya madirisha ya chini ya treni yalivunjwa.
Mkazi mmoja wa eneo la jirani amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba "Tulisikia kishindo kwanza na baadaye, kikali zaidi,"na "Baadaye tukasikia watu wakipiga kelele. Hali haikuwa nzuri."
Uchunguzi kadhaa umefunguliwa kuhusu tukio hilo, ikiwa ni pamoja na ProRail - chombo cha kiserikali kinachohusika na mitandao ya reli nchini humo.




