Taarifa ya uamuzi huo inasema Syria inaweza kuanza tena ushiriki wake Mikutano ya Umoja wa Kiarabu mara moja, huku ikitoa wito wa azimio ya utatuzi wa mgogoro unaotokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, ikiwa ni pamoja na watu kulikimbia taifa hilo kwenda nchi jirani na kadhia ya ulanguzi wa dawa za kulevya eneo lote la kanda.
Akitoa tangazo hilo jioni ya jana Jumapili, Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit amasema matarajio yake ni kwamba mataifa mengi ya magharibi yanaweza yasifurahishwe na uamuzi wao huo huo wa lakini huo ni uamuzi huru wa mataifa ya Kiarabu ambao unaona kwamba maslahi yao yanahitaji, kwa wakati huu mahususi, kutoliacha suala la Syria kwa namna lilivyoendelea kuwa.
Wakati mataifa ya Kiarabu ikiwa ni pamoja na Umoja wa Falme za Kiarabu kushinikizwa kusimamisha mara moja hatua ya kutengwa kwa Rais Assad, baadhi wamepinga hatua hiyo pasipo kuwepo kwa suluhu ya kisiasa kwa mgogoro wa Syria, ikiwa kama sharti muhimu la Syria kuridhiwa kurejea katika jumuiya hiyo.