Wednesday , 5th Jul , 2023

Katibu mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Felchesmi Mramba ametembelea banda la Maonesho la Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba, na kushuhudia rekodi za kipekee zilizowekwa na kampuni hiyo

Katika maonesho hayo, GGML inajivunia kushiriki kwa mara nyingine tena huku ikiwa imenyakua tuzo ya Kimataifa ya masuala ya Usalama kazini (Global Safety Awards) pamoja na utekelezaji wa miradi kemkem ya inayoinufaisha jamii ya Watanzania.

Maonesho ya Saba Saba ambayo ni fursa kwa Tanzania kushuhudia matunda ya mafanikio yaliyotekelezwa katika nyanja mbalimbali pia yanatajwa kuwa fursa ya kusherehekea maendeleo ya sasa na kuangalia malengo ya taifa ya baadae