Saturday , 28th Jun , 2025

Watu wanne ambao bi wakazi wa kijiji cha Mtegu wilayani Lindi wamefariki dunia kufuatia ajali ya gari yenye namba za usajili T157 EAV iliyokuwa inatokea mkoani Ruvuma kuelekea Mtwara kuacha njia na kuwagonga wakazi waliokuwa wamekaa kwenye makazi yao.

Ajali hiyo imetokea usiku wa tarehe 27 ambapo akizungumza kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Lindi Kamishna msaidizi wa polisi John Imori amesema mara baada ya kusababisha ajali hiyo dereva amekimbia na juhudi za kumtafuta zinaendelea huku akieleza kuwa uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo unaendelea.

Aidha akizungumza mmoja wa wakazi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa Jina la Karimu Salumu ambaye katika ajali hiyo amempoteza baba yake mzazi amewaomba medereva kufuata sheria za barabarani huku akiitaka serikali kuchukua hatua ya kuweka tuta katika eneo hilo ili kunusuru kutokea kwa ajali zaidi.