Monday , 30th Jun , 2025

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amelihutubia Bunge Ijumaa ya Juni 27 ambapo pamoja na hotuba hiyo alitangaza tarehe ya kuvunjwa Bunge rasmi kuwa ni Agosti 3, 2025, kwenye hotuba yake Rais Samia aliweka bayana mambo muhimu ambayo ameyatekeleza kwenye kipindi

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amelihutubia Bunge Ijumaa ya Juni 27 ambapo pamoja na hotuba hiyo alitangaza tarehe ya kuvunjwa Bunge rasmi kuwa ni Agosti 3, 2025, kwenye hotuba yake Rais Samia aliweka bayana mambo muhimu ambayo ameyatekeleza kwenye kipindi chake ikiwemo;

Ukusanyaji wa kodi kutoka TZS 1.51 trilioni mwaka 2020 mpaka TZS 3.09 trilioni mwaka 2025 ikiwa ni sawa na ongezeko la 104%, umimarishaji wa mifumo ya utoaji haki na ujenzi wa vituo vipya vya kote nchini.

Si hayo tu kwenye kipindi chake Rais Samia amejinadi Kuongeza Fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu (Boom) kutoka TZS 7,500 hadi TZS10,000 kwa siku za masomo sawa na ongezo Chanya la 33.33%, Pia thamani ya mikopo ya elimu ya juu HESLB kutoka TZS 464 bilioni hadi TZS 786 bilioni sawa na ongezeko chanya la 69.4% na kunufaisha wanafunzi 229,000.

Katika mifumo ya utoaji wa haki nchini Rais Samia amejinasibu kwa uteuzi wa majaji wapya 83 na kuajiri mahakimu na watumishi wa mahakama 1,153 na upatikanaji wa haki kwa wakati na kupunguza msururu wa kesi mahakamani.

pasipo kusahau Rais Samia amejinasibu kuwa katika wakati wake uhuru wa vyombo vya habari na watu kutoa maoni umeimarika ukilinganisha na utawala uliopita.