
Baadhi ya watumiaji wa kitoweo cha Nyama katika Manispaa ya Mpanda Mkoa wa katavi wameziomba mamlaka zinazohusika kuingilia kati ongezeko la bei ya nyama kutoka 10000 hadi 12000 kwa kilo moja.
Wakizungumnza na EATV wakiwa kwenye mabucha ya nyama wananchi hao wamesema ongezeko la bei hiyo linawafanya kushidwa kumudu bei hiyo ya kitoweo cha nyama.
''Elfu kumi na mbili jamani wengine hatuna uwezo, huo wito wangu kwa serikali mama samia ni mwanamke kama sisi tuangalie jamani hali ni ngumu tunashidwa kununua nyama" Anasema Jesca Samweli mkazi wa Mpanda.
Kwa upande wake, Abdallah Thabiti Waziri ambaye ni Afisa mfawidhi bodi ya nyama kanda ya Magharibi amesema wao kama bodi ya nyama hawana mamlaka ya kuzuia bei hiyo ingawa hutoa ushauri kwa watoa huduma ya nyama ili wananchi waendelee kupata huduma bila kuathiri watoa huduma hao kulingana na gharama za uendesheshaji wa biashara zao.