Simba waingia kambini,Berkane kutua kesho Dsm
Klabu ya Simba imeingia kambini leo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa makundi kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Rs Berkane ya Morroco kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa siku ya jumapili saa kumi kamili jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

