Barcelona yaweka rekodi Italia, yafuzu 16 bora
Klabu ya FC Barcelona imefuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya UEFA Europa League kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-3 dhidi ya Napoli, hii ni mara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 jana usiku kwenye mchezo wa mkondo wa pili hatua ya mtoano. Na Droo ya hatua ya 16 bora inafanyika leo.

