Polisi wataja majina ya waliofariki ajalini Kagera
Watu wanne wamepoteza maisha baada ya gari la mizigo walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka, Desemba 23 mwaka huu, majira ya saa 03:00 asubuhi, katika mteremko wa Kishoju, Kata ya Kihanga wilaya ya Karagwe, mkoani Kagera.