Wanafunzi wasio na sare wasizuiliwe shuleni
Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu, amewataka wakuu wa shule wasiwazuie wanafunzi kuanza masomo pale wanapokuwa hawana sare za shule, bali watoe muda kwa wazazi walau wa mwezi mmoja ili waweze kuwanunulia watoto wao sare.