Baba avunja shingo na uti wa mgongo wa mwanaye
Jeshi la polisi mkoani Kagera, linamshikilia Amos Rudovick (39) kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mtoto wake Dastan Amos (13), kwa kumchapa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na baada ya uchunguzi ilibainika kuwa alimvunja shingo na uti wa mgongo.