Tamasha kubwa la wanamuziki kutoka Afrika ya Kusini, Liguideep na Mi-casa ambao waliletwa nchini na na kampuni ya Black Sensation wakishirikiana na Juega casa, lilifanyika katika viwanja vya Sea Cliff Hotel , Novemba 2013.

Tamasha hili kubwa liliacha historia ya aina ndani ya mwaka 2013, lilidhaminiwa na redio kali inayopendwa na wengi hapa Tanzania, East Africa Radio.

Novemba, 2013 chini ya ushirikiano mkubwa wa Black sensation na Juega casa, East Africa Radio waliweza kuwaburudisha wapenzi wa kwaito nchini kutoka sehemu mbalimbali baada ya kuwaleta wasanii hao na kutumbuiza kwa takribani masaa matatu.

Wapenzi wa burudani walijitokeza wengi sana kwenye viwanja vya Sea Cliff Hotel, na kufanya iwe burudani ya Taifa maana umati wa watu waliojitokeza ulikuwa ni mkubwa sana.

Mashabiki hao waliojitokeza kwenye tamasha la Black Sensation 2013, waliweza kukwapua zawadi mbalimbali ikiwemo Tshirt , albamu za wasanii hao na vitu vingine mbalimbali.