Ulikua ni usiku mnene pale kundi la wasanii kutoka nchini Nigeria Psquare walipowasili nchini na kutoa shoo ya kihistoria.

Psquare linaloundwa na mapacha Peter na Paul walitinga show hiyo 23 Novemba 2013.
kikundi hiki amabacho kina umaarufu mkubwa barani Afrika na mabara mbalimbali ulaya, linatamba zaidi kwa kuwa na nyimbo zenye lugha,beats na biti za Kiafrika. kundi hilo pia linatamamba kwa kuwa na video kali za dansi.

Chini ya udhanini mkubwa wa kampuni ya simu ya vodacom, p square walipagawisha mashabiki wao kwa kuimba nyimbo mbalimbali za zamani na sasa na kutoa burudani mbalimballi , wasanii hao pia walitoa vituko mbalimbali vilivyovunja mashabiki mbavu.

katika tamasha hilo wasanii hao walionyesha kufurahishwa na mapokezi waliopata kutoka Tanzania na kuwapa changamoto mashabiki nchini wakiwasii kuwapenda wasanii wao ili waweze kukua na kufikia kiwango chao.

Wasanii hao walitembelea kituo cha watoto yatima na kutoa misaada mbalimbali pamoja, vile vile walitembelea studio za televisheni ya East Afrika televisheni na redio na kufanya mahojiano katika vipindi mblimbali na kuwashukuru mashabiki wao.

Tamasha hilo lilishuhudiwa na mashabiki mabli mbali wakiwemo wakigeni na wakazi wa jiji la Daresalaam waliofika katika usiku huo wa kihistoria.

P square wakionyesha mashabiki vipaji vyao vya ziada na ujuzi wa matumizi ya vyombo vya muziki.