Kundi la wasanii kutoka Afrika kusini lijulikanalo kama Mafikizolo waliwasili nchini na kutoa burudani kali kwa wapenzi wa miondoko ya kwaito.
Kundi hilo liundwalo na mwanadada Nhlanhla Nciza na Theo Kgosinkwe walitumbuiza katika ukumbi wa Mlimani city Hall Aprili 5, 2014 .
Kundi hili linalojivunia umaarufu mkubwa wa afro pop kutokana na vibao vyao vingi kuchezwa sana kwenye hafla mbalimbali kund hili limeibukia umaarufu zaidi pale nyimbo zao mpya kama Khona na Happy kukonga nyoyo za mashabiki wengi zaidi barani Afrika.
Tamasha hili lilifanikishwa chini ya udhamini mkubwa wa makampuni ya vinywaji Hennesy, Castle Lite, Pepsi pamoja na East Africa Television (EATV) pamoja na East Africa Radio.Mafikizolo walitoa burudani mwanana kwa kuimba nyimbo mbalimbali zilizotamba zaidi awali na kumaliza tamasha kwa nyimbo zao maarufu zaidi kwa sasa, wasanii hao pia walionesha umahiri wao wa kucheza dansi mbalimbali zilizopagawisha mashabiki wa miondoko ya kwaito na Afro house.
Katika tamasha hilo wasanii hao walionyesha kufurahishwa na mapokezi waliopata kutoka Tanzania na kushukuru mashabiki kwa kuwaimbia nyimbo mbalimbali za shukrani kwa lugha ya Xhosa.
Mafikizolo walitembelea studio za televisheni ya East Afrika televisheni (EATV) na East Africa Radio na kufanya mahojiano katika kipindi cha Friday Night Live (FNL) na kuwashukuru mashabiki huku wakionyesha staili zao za kudansi..
Licha ya kua hawajui kiswahili wasanii hao walijifunza maneno machache ya kiswahili kushukuru mashabiki pamoja na kutafsiri nyimbo zao mbalimbali ili kufikisha ujumbe halisi kwa mashabiki wao.