Msimu wa pili wa mashindano makubwa ya kucheza Africa Mashariki Dance 100% mwaka 2013, yalilitikisa jiji la Dar es Salaam na Tanzania nzima kwa ujumla baada ya makundi yenye ujuzi mkubwa kujitokeza.

Baada ya mchujo kufanyika, makundi matano yaliyopita na kufanikiwa kwenda kwenye fainali ni kundi la The chocolate, DDI Crew, Wakali Sisi, The Winners na The WT.

Makundi yote yalipewa muda wa kujianda vizuri ili kuonesha uwezo wao mkubwa, maana makundi yaliyoingia fainali yalikuwa yana uwezo mkubwa katika uchezaji, hali iliyofanya hadi majaji kuwa makini sana katika kuamua.

Baada ya vuta nikuvute nyingi, hatimaye alipatikana mshindi kwa 2013, na kundi hili lilijulikana kwa jina la 'The Chocolate' toka jijini Dar es Salaam.

Mabingwa wa Dance 100% (2013) kundi la The Chocolate, wakikabidhiwa cheki yao ya Tsh. MILLIONI TANO na kombe la ubingwa kutoka kwa Mkuu wa Chapa na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Bw. Kelvin Twissa.